Barua Kwa Kizazi cha P.O.Box

My Writings

Salam Kwenu (Shikamooni)

Binafsi naendelea Vizuri na afya, nalisukuma gurudumu la maendeleo kwa kuifanya leo yetu mlio iita “KESHO YA WATOTO WETU” iwe njema ili kesho ya wajukuu zenu ikawe na matumaini. Si mlisema “WATOTO NI TAIFA LA KESHO?” Kesho yetu imewadia na ni ngumu haswa na nihapa ndipo nimkumbukapo “Sijui Mhenga gani aliye sema  (Kuwa Uyaone)” ila kikubwa ni kushukuru kwa malezi yenu mliyo tupa na sasa tunajivuna kuitwa #Wantanzania.

Neno langu Watanzania nimeliwekea alama # na yawezekana hujafahamu maana yake ingawa wengi huita alama ya reli. Si lengo langu kukupa somo juu ya alama hii ila lengo langu haswa ni kukupa Shule ambayo pengine Mtoto wako umuitaye kizazi cha Dot (.) Com hajakufahamisha. Mambo muhimu ambayo leo nimeona nivyema niyazungumze japo kwa uchache wake. Najua huwezi choka kusoma kwasababu kizazi chenu ni tofauti na chetu. Enzi zenu mlikuwa mnapenda kuandika” Barua ndefu kama hii”, Natena mlikuwa mnapenda kusoma haswa, ubaya ni kwamba hamkupandikiza mbegu mwanana kwa sisi vijana wenu na ndio maana tunapuuzia maandiko kama haya.

Niende kwenye lengo la Barua Hii.

Mpendwa Baba, Mama, Mjomba, Shangazi na kadharika. Tupo kwenye ulimwengu ambao kwa namna moja ama nyingine mmetuandalia, bahati mbaya ni kwamba “Teknolojia” na maarifa haya hamkuyapata na zaidi miaka ya 2000 mliita kipindi cha Y2K, wengi wenu mliona ni kupoteza muda kujishughurisha na Mambo ya barua pepe kipindi hicho mlitumia Hotmail na Yahoo na mitandao ya kijamii ilikuwepo kwa uchache wake hapa nazungumzia miaka ya 2005 na kadharika.

Huwa ninapitia pitia kurasa zenu za Mitandao ya kijamii na muyawekayo humo hunifanya nitabasamu.  Somo langu kwenu ni hili, KILA UKIWEKACHO KATIKA INTERNET WATU WOTE WANAONA, zaidi kitadumu kwa miaka mingi. Hapa simaanishi picha za utupu na kadharika ambazo vijana na watoto wetu wanaweka kila kukicha.

Hapa ninamaanisha Maandiko, Comments, Likes na kila picha uiwekayo katika Facebook Page yako itakuwepo tu. Yani miaka Kumi ijayo Kitukuu chako kikitaka kutizama Swagga za babu yake miaka kadhaa nyuma ataona.

Kwanini Nimeandika??  Nifananishe zama hizi na zama za ALBAMU na picha mlizo kuwa mnapiga kwa kila aina ya POZI, na miaka kadhaa baadaye mmekuwa mkituonesha namna mlivyo ishi nasi hufurahia hayo yote huku tukisema wazee walikuwa “MAJEMBE” hapa ninamaanisha walikuwa watu makini na kila picha ina maelezo yenye ujumbe mwanana ndani yake.

Miaka kadhaa ijayo hatuto tumia albam tena, badala yake tutatumia Kurasa zenu za mitandao ya kijamii kushare na wanetu na wajukuu Habari zinazo kuhusu. Wakitaka kukufahamu, namna ulivyo kuwa unaongea, una-reason na kadharika watatumia Maandiko yako, post zako na kila kitakacho onekana waki-Google au Ku-Facebook jina lako.

Wengi wetu hatufahamu haya, sasa imagine kipindi kile ulipo kuwa unapiga picha na kuzihifadhi kwenye Albamu, ndio ungekuwa unapiga picha za sisimizi, au unajaza picha za kwenye magazeti cha Nyerere na Mwinyi kama rasi, Natena wa wakristu albamu nzima ungekuwa umejaza Picha za Yesu na mama maria, Kwa waislam na madhehebu mengine mkafanya hivyo hivyo, sidhani kama albamu zingetazamika.

Ninacho maanisha ni hiki, Hizo kurasa zenu ni sehemu za kuandika au kushare mambo ambayo utapenda ukumbukwe nayo kwasababu hakuna namna dunia tuishiyo ndivyo itakavyo. Kwa uwepo wa smart phone mtu unajikuta nilazima uwe na Barua pepe ambapo hapo mwanzo zilionekana hazina Maana, ili uweke CV zako za kazi mahala Fulani wanakutaka uwe ni ukurasa wa Linked In na kurasa nyingine za kijamii.

Basi ni muda muafaka wa Kujifunza namna Sahihi ya Kuandika katika kurasa zako za kijamii. Masomo yatakayo fuata yataelezea kwa kina namna ya kuyafanya haya.