Kufeli liwe ni Darasa ili uwe Muhitimu Bora

“Dad! Why Do You Watch the Same Cartoon Over and Over Again?”

Nikamuangalia usoni na kutabasamu, Moyoni nikajisemea:

“Yani wewe! Maswali kama Mamako, Ungejua ninavyo usaka Ugali kwa kila namna, ungetamani kuomba Poo!”

Nikamjibu:

“Ni vile nafurahishwa na Mr. Moon anavyo feli katika mipango yake na baadae anafaulu.”

Akajibu:

“OK Dady! Mi napenda Mr Moon anavyo osha gari amevaa Under Pant”

Akacheka mpaka jino la mwisho likaonekana, Kisha akamvuta mdogo wake na Kuelekea nje kucheza.  Huyo alikuwa ni Caspar, mwanangu wa Kwanza.  Nilimtizama na kujisemea:

“Hakika nimekuwa mtu mzima, natamani WAZAZI Wangekuwepo ili wajionee wajukuu wao walivyo wakubwa, wenye busara na hekima” na namwomba Mwenyezi Mungu hekima hizi ziendelee mpaka ukubwani, maana Dunia ilivyo kaa  Sometime unatamani isimame ili ushuke uhamie Sayari nyingine.”

Lengo La Andiko: Sijatamani kusubiri sana katika kuliandika hili lililo nijia leo. Cartoon ya “SING” ni animation ambayo binafsi huwa sichoki kuitazama. Leo nikiwa mitaa Fulani Napata Maarifa Professor husika wa somo ametumia Cartoon hii katika somo lake na pia akatumia series ya “Game of Throne” katika kufundishia.

Nimejikuta nacheka sana nahata baadhi ya wanafunzi wangu kadhaa watacheka KOZ hiki si kipya kwangu. Mara kadhaa nimeitumia Cartoon hii ya Moon katika kufafanua baadhi ya mambo na kukuta huyu mdau akiitumia kumenifurahisha nakujikuta nimekuwa “bonge la Profeseri”

Any way Cartoon ya “SING” ina mhusika aitwaye MOON, Jamaa mwenye Ndoto kubwa, na anatumia kila awezalo kama Mjasiriamali kuhakikisha ndoto Zinatimia. Kila hatua ya Cartoon hii ni funzo kwa mjasiriamali awe ni wa Tanzania au popote pale duniani.

Zaidi Moon anaonesha njia kadha wa kadha katika kutafuta mitaji au mtaji ili kuweza timiza malengo. Wawekezaji wanapo kataa na kuto ielewa nia au lengo lako haimaanishi ndoto na mawazo yafe. Ndugu na jamaa wanapo kataa kusapoti ndoto zako haimaanishi Ndoto hizo zife, Zaidi ni kuelewa  ni kwanini wamekataa au wameshindwa kusapoti. Kuwa mwepesi wa kukubali, kushukuru inapo bidi na kusonga mbele.

Nafahamu kuna maandiko mengi umesoma na unasoma, na sometime inaboa kusoma tena na tena kitu au swala lile lile. Na ndio maana napenda kuandika yale yanayo nihusu ili kuweka kautofauti Fulani.

Binafsi nimekuwa nikiwa na kila Tamaa ya kufanikiwa. Sikuwahi na sijawahi kuwa na MOJA TU katika nifanyayo, na nimefeli mengi katika maisha huku nikijipa Moyo kwamba nitafanikisha tu. Kigumu katika safari hii ni ku-Admit kwamba nimefeli. Kwangu ninauita “MTIHANI” yaani kufeli na kukubali kama nimefeli.

Nikapata bahati ya kutembelea “Innovation Center” hapa ni mahala maalumu ambapo Investors, Developers, Designers na wadau wengine hukutana kwa ajili ya kujadili Mawazo au Ideas ili ziweze kwenda Next step. Nimekutana na wengi na nimejifunza mengi. Nimekutana na watu walio feli zaidi ya mara tano nabado wana imani ya kufanya tena na tena pasipo kujali watafeli mara ngapi.

Wamekula na wanakula kiapo cha kuto kata tamaa mpaka kieleweke. Nami nikajikuta naingia katika jumuiya hiyo ya kula kiapo cha kuto kukata tamaa. Kwa wanao nifahamu nilianza na Ndoto ya kuwa mtunzi, nikitamani kuandika kitabu changu cha kwanza cha riwaya nikiwa sijazidi miaka 18, Nikafeli.

Nikaanzisha Startup yangu ya kwanza ikiitwa “RAMANI TANZANIA” na sapota wa kwanza akiwa ni My fiancé by then na sasa mke wangu XXXX pia Musa Gunda ambaye alikuwa ni mwana funzi wangu na rafiki, Nikaja na “Academify – Nikafeli ”, Niwezeshe Crowdfunding website – Nikafeli, na kadhalika kibao.

Kumbe Kufeli au kushindwa ni darasa. Ni darasa lenye kutoa kila aina ya mafunzo, muhusika hana budi kujifunza kadri siku zinavyo songa mbele. #MpakaWakatiMwingine