Matokeo Ya FORM FOUR na Hatima Yangu (Maalumu kwa Wanafunzi na Wazazi)

My Writings

Naamka asubuhi nikiwa na haraka zangu, Kichwa kikiwa kizito kutokana na Shughuri za Jana. Mara PAAAAP!!! Napokea simu Kutoka kwa Mwanafunzi wetu Julieth kutoka Jangwani akiwa anahema kwa pasipo kuweka kituo nami sikusita kuuliza KULIKONIIIII?

“Matokeo Yametoka!!”

Nikamuuliza, “Unasema?”

Naye bila ya Ajizi akajibu, “Yametokaaa, nashindwa hata pakuanzia!”

Kufanya Stori hii kuwa fupi nikwamba, Matokeo ya form four ndo hayo yametoka, Kila mmoja anapanda kile alicho kivuna. Binafsi haka kamsemo huwa sikapendi ila ndio hivyo tena, Ukweli Mchungu na hatuna budi kuvumilia.

Je! Matokeo yako au ya mwanao yametokaje?

Kwa uzoefu wangu na baadhi mtanisaidia, Hapa ndipo maisha ya kijana wako au wewe muhitimu wa kidato cha nne huanza, na nihapa ndipo penye kuhitaji umakini katika kufanya maamuzi kwa wewe kama Mzazi au wewe kama Kijana.

Baadhi yetu wahitimu wa form four mpaka jana asubuhi wakati Matokeo yalipo kuwa yakitangazwa hatukuwa na plan B wala C. Mara yalipo tangazwa ndio zile Akili ya kukurupuka zinakuja na kuanza kupanic hasa baada ya kuona Mavuno ya ulicho panda, na baadhi hatujawahi kuwa na Plan ya maisha tukidhani Sisi niwatoto kila siku.

Baadhi wame/Walijiongeza na kuanza harakati kadha wa kadha na matokeo yametoka, hawajashtushwa sana na Mavuno yao.

 

Labda niende kwenye OPTION ninazo ziona ambazo ninaziandika kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi na Watoto/Vijana.

 

Kuna walio pata Division One na Two. Hawa binafsi sinto wazungumzia sana kwani kwa asilimia kubwa wananafasi tena kubwa ya kuendelea na Kidato cha tano huku wakiwa na uwanja mpana wa kichagua Combination.

Division Three: Hapa kuna wenye Credits ambazo zinaleta Combinations Fulani za masomo na nidhahiri kwamba form four kwao ni Mtelezo.

Kuna wale ambao wana DIVISION THREE ambazo hazija balance, Baadhi wanatamaa ya kuendelea na Form FIVE ila ndio hivyo tena, Combinations hazija kubali. Huamua kurudia form four au kwenda Pre-Form Five ili matokeo yakitoka ya mtihani atakao rudia basi aunganishe form Six.

Maumivu huja baada ya kurudia mtihani, wazazi kulipa ada nabado Akakosa Credit ya kumfanya aendelee. FRUSTRATION huanzia hapa. Kisaikolojia huyu hatokuwa sawa kwa muda, Familia itapoteza Imani kwake, Marafiki wa zamani na wapya watamwona Kilaza, nayeye binafsi atajiona asiye na akili za darasani.

Kuanzia hapo hata ile ya kujiamini akiwa peke yake hupungua, ataishia kuandika Status za kila aina Akikariri mistari ya kwenye Biblia kuonesha KILA KITU KIKO SAWA, ata Quote maandiko kutoka kwa wanazuoni kadha wa kadha au watu walio fanikiwa pasi kuwa na elimu  nahata mifano yake ya maisha ataitumia ya watu hao ili tu kuonesha kwamba kila kitu kiko sawa. Jibu ni HAKUNA KILICHO SAWA!!

Kuna wale wenye matokeo mazuri, Credits nzuri, ila tatizo lipo kwenye uchaguzi wa Combination ya kwenda kusoma au Kwenda kusoma asicho kitaka. Hili nalo Janga. Hapa napo pana changamoto kubwa haswa na matokeo yake ni Ile ile FRUSTRATION mara baada ya Matokeo ya form SIX kutoka.

Ni mara ngapi Tunaona watu walio pata DIVISION ONE, TWO na THREE nzuri kabiza form four wakipata ZERO au Four Kidato Cha SITA?

NINI KIFANYIKE KWA WAZAZI NA WANAFUNZI?

Kwa wanao taka kwenda Form Five:

  1. Fanya Chaguo Sahihi la Combination ili uweze kwenda High School ukiwa na Malengo. Combination hiyo iwekee malengo na anza kufanya research/Utafiti sasa kwamba ukisoma hiki unaweza kuja soma Hiki na kile chuo kikuu na baadaye ukawa Fulani au fanya kazi ya aina Fulani.
  2. Kama akili yako haiku OK na wazo la Kwenda High School kuwa muwazi kwa mzazi mapema. Wengi mnatabia ya kuficha au kuogopa na matokeo yake mkifika shule hamsomi mkidhani mnamkomesha mzazi. Nasi wazazi tuwe wepesi wa Kusikiliza, Zaidi tuzifanyie tafiti shule wanazo enda watoto wetu hasa hizi za Private. Fungua necta.go.tz na angalia matokeo ya Miaka ya nyuma kama Yanaridhisha.
  3. Kama ni chuo BASI kitembelee au zungumza nao kwenye simu. Fahamu Options zilizopo kwa mtoto kusoma hapo na kama CHUO husika kimesajiriwa na Mamlaka husika.

Kwa wanao RISITI au kufanya upya Mtihani Upya. Mzazi au mwanafunzi ni vyema akajiuliza mara mbili mbili juu ya nikwanini anaamua Kurudia Mtihani. Zaidi ajipime kwa kina kuona kama anacho kifanya ni sahihi na kama yupo tuyari kusoma kwa bidi ili aweze kurudia mtihani.

KWA Wanao Taka kusoma VYUO.

Mara baada ya kupata matokeo, OPTION ambayo ninaiita ni STRESS free ni kuamua kujiunga na Chuo. Serikali imeruhusu Utaratibu huu ila Zingatia yafuatayo.

Mpaka Mwaka huu 2019, Vyuo vya serikali vilivyo sajiriwa na NACTE vinapokea walio maliza form four na ukasoma KOZI ya Mwaka Mmoja, Then ukasoma DIPLOMA kwa miaka Miwili Mpaka Mitatu na kisha UKAOMBA MKOPO na kujiunga na CHUO kikuu yaani Degree.

Vigezo vipo tofauti tofauti. Mfani Ukitaka kusoma Information Technology ngazi ya CHETI  ili uweze kuendelea na DIPLOMA ya Masomo ya COMPUTER Na DEGREE hapo baadaye basi unatakiwa uwe na PASS za form four NNE. Yaani uwe na D, C, B au A katika masomo manne na katika masomo hayo usihesabu Somo la DINI.

Kozi nyingine hususani za Afya zinaruhusu Pass Tatu ila ni vyema ukawasiliana na Chuo.

Kama hauna PASS nne na unatamani kuendelea na Shule basi waweza kurudia mtihani ili upate PASS au unaweza anza na VETA ambapo utapata Grade 1,2 na 3 Kisha utajiunga na CERTIFICATE ili upate Grade 4 na Utaendelea na Diploma kisha kuzifikia ndoto zako za Degree.

 

NLab Innovation Academy

Tunatoa DIPLOMA / CERTIFICATE Za Information Technology

Tupo: Kinondoni, Vijana Mtaa wa MAFERE.

Email: admissions@nia.ac.tz

Website: www.nia.ac.tz

Wilhelm Caspar Oddo

Piga au tuma Meseji hapa: 0744100231