Nafasi Za Kazi Maalumu(31) Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoa Wa Tabora

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora Inapenda kutangza nafasi za kazi kwa watanzania wenye sifa zifuatazo:

MKUSANYA USHURU NAFASI-31:

SIFA ZA MWOMBAJI:

 • Lazima awe Mtanzania
 • Awe na elimu ya kidato cha nne
 • Awe mwaminifu

KAZI NA MAJUKUMU:

 • Kukusanya mapato kutoka  katika vyanzo vya Halmashauri.
 • Kutunza Kumbukumbu za hesabu.
 • Kupeleka fedha alizokusanya benki kilasiku.
 • Kufanya kazi nyingine atakazo pangiwa na mkuu wake wa kazi

MASHARTI YA JUMLA:

 • Awe amehitimu na kupata cheti cha taaluma cha kidato cha nne (iv)
 • Awe na cheti cha kuzaliwa
 • Barua zote za maombi ziambatane na nyaraka zifuatazo;

-Nakala za vyeti vya mwombaji vilivyothibitishwa.

-Maelekezo binafsi ya Mwombaji(curriculum vitae).

-Barua ya Mdhamini.

-Picha Ndogo za rangi(coloured passport size mbili(2) za hivi karibuni.

 • Kila mbombaji lazima awe na umri kati ya miaka  18-45
 • Barua ambazo hazikuambatanishwa na nyaraka hapo juu(i-iv) hazijafanyiwa kazi.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:

MKURUGENZI MTENDAJI,

HALMASHAURI YA WILAYA,

S.L.P.19,

iGUNGA.

Mwisho wa kupokae maombi ni;

Tarehe: 09/09/2021, Saa 9:30 alasiri

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *