Fulsa Ya Mitaji Kwa Wanavikundi Kutoka Makundi Maalum, Vijana, Wanawake, Na Walemavu Wa Manispaa Ya Halmashuri Ya Wilaya Ya Kinondoni-Dar Es Salaam

 

 

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI NI MOJA KATI YA HAKMASHAURI TANO(5) ZINAZO UNDA  MKOA WA DAR ES SALAAM. ZINGINE NI HALMASHAURI YA YA MANISPAA YA TEMEKE, UBUNGO, KIGAMBONI NA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI ILIANZISHWA KWA SHERIA YA SERIKALI (MAMLAKA ZA MIJI) SURA YA 288 KUPITIA TANGAZO LA SERIKALI (GOVENMENT NOTICE NO.4) YA MWAKA 2000 N AOFISI YA RAISI, TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA KAMA CHOMBO HURU, HIVYO KUPITIA MAMLAKA YA KUONGEZA UBORA WA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI WAKE.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA  YA MANISPAA YA KINONDONI ANAPENDA KUVITANGANZIA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA, NA WATU WENYE ULEMAVU VILIVYO NA SIFA ZA KUPATA MIKOPO ISIYO NA RIBA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022, KUWA MANISPAA IMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO HIYO ISIYO NA RIBA, KIASI KILICHOTENGWA NA SERIKALI KWAAJILI YA MIKOPO HIYO ILIYO TENGWA NI 3,978,903000 SAWA NA 10% YA MAPATO YA NDANI YA MANISPAA. HIVYO MNAOMBWA KULETA MAOMBI YA MIKOPO, MAOMBI HAYO YAANZA NGAZI YA MTAA, KATA NA HATIMAE YAHAKIKIWE NA AFISA MAENDELEO JAMII NGAZI YA KATA KISHA YAPITISHWE NA KAMATI YA MAENDELEO MGAZI YA KATA
MCHANGANUO WA FEDHA ZILIZO TENGWA KWA VIKUNDI NIKAMA IFUATAVYO:
 • VIKUNDI VYA WANAWAKE: 1,591,561,200
 • VIKUNDI VYA VIJANA: 1,591,561,200
 • VIKUNDI VYA WATU WENYE ULEMAVU: 795,780,600
VIGEZO:
 • KIKUNDI KIWE KIMESAJILIWA
 • KIKUNDI KIWE NA KATIBA INAYOONESHA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA KIKUNDI
 • KIKUNDI KIWE NA MRADI AU MIRADI NA SEHEM MAALUMU INAYOTAMBULIKA YAKUFANYIA SHUGHULI ZAO.
 • UMRI WA VIKUNDI VYA VIJANA NI KUANZIA MIAKA 18-35
 • KIKUNDI LAZIMA KIWE NA AKAUNTI NAMBA YA BENKI KWAAJILI YA KUPITISHIWA MIKOPO.
 • IDADI YA WANACHAMA WA VIKUNDI VYA WANAWAKE NIKUANZIA WA 5 NAKUENDELEA, WALEMAVU NIKUANZIA WA2 HADI WATU WA5
VIAMBATANISHO:
 • NAKALA YA CHET CHA USAJILI WA VIKUNDI.
 • SLIP YA BENKI INAYOONYESHA AKAUNTI NAMBA YA KIKUNDI
 • MIHTASARI YA KIKAO CHA KIKUNDI YENYE AGENDA YA MIKOPO
 • FOMU YA MAOMBI YA MIKOPO (INAYOPATIKANA OFISI YA KATA HUSIKA)
 • MCHANGANUO WA MRADI ULIO OMBEWA NA KIASI CHA MIKOPO
 • NAKALA YA KITAMBULISHO INAYOONYESHA UMRI WA VIKUNDI VYA VIJANA
WOTE WENYESIFA MNAKARIBISHWA
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE:30 DISEMBA 2021 SAA 9:30 ALHASIRI

Kwa maelezo zaidi Tembelea

http://www.kinondonimc.go.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *