Call For Work At Benjamin Mkapa Foundation (BMF) (various posts)

Overview
The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF) is a non-profit Trust, established in 2006 with the vision towards healthy lives and well-being for all, in Tanzania and the rest of Africa. Its strategic focused results areas include to combat HIV and AIDS, TB, Malaria and Reproductive, Maternal New Born, Child and Adolescent Health coupled with Health Systems Strengthening including Human Resource for Health. The Foundation addresses the above health challenges through innovative design and implementation of sustainable programs such as the Mkapa Fellows Program.
The achievement of the BMF’s vision can be achieved through an empowered workforce, which is self-motivated, committed to growth and integrity, and seeks excellence in execution.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) inatekeleza Mradi
wa Kuimarisha Mifumo Stahimilivu na Endelevu ya Afya (RSSH) kupitia
ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na
Malaria (Global Fund). Mradi huu una lengo la kuimarisha huduma za afya
katika Mikoa kumi (12) iliyopewa kipaumbele na mradi huu.
Wizara inapenda kuwatangazia wataalamu wote walioomba nafasi za kazi za
Kada mbalimbali za Afya, kupitia mfumo wa Kielektroniki wa maombi ya
kazi wa Wizara ya Afya kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi
kupitia ufadhili wa Global Fund chini ya Taasis ya Mkapa umekamilika hivyo
wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia
maelekezo yafuatayo kabla ya kwenda kuripoti katika vituo:
i) Kuhudhuria kikao kazi kwa ajili ya kujaza mikataba ya kazi na
kukamilisha taratibu za ajira siku ya Tarehe 5 ya Mwezi wa 10 Jijini Dar Es
Salaam (Ukumbi Mtajulishwa).
ii) Aidha waombaji watakaoshindwa kufika katika kikao kazi tajwa hapo juu,
nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka iwezekanavyo ndani ya
siku Kumi na nne.

iii) Wataalamu waliopangiwa kazi wanahitajika kufika wakiwa na nyaraka
zifuatazo: –
a. Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne/Sita
b. Nakala ya vyeti vya Taaluma
c. Cheti halisi cha usajili na leseni kwa kada zinazohusika kama vile;
wateknolojia na wauguzi.
(Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mkuu) 40478 DODOMA.

Fax Na: S.L.P. 743,
Namabari ya Simu: +255 026 – 2323267 Barabara ya Afya,
Telegram “AFYA”, DODOMA Mji wa Serikali Mtumba,
d. Cheti cha mafunzo kwa vitendo (internship)
e. Cheti halisi cha kuzaliwa.
f. Nakala ya kadi yako ya benki.
g. Nakala zote za vyeti vilivyotajwa hapo juu viwe vimepitishwa na
mwanasheria ili kuthibitisha kama ni nakala halisi za mwombaji.
h. Maelezo binafsi (CV) ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya
simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya
wadhamini wako wasiopungua watatu (3).
i. Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti.
Orodha ya majina ya wataalam wote waliopangiwa vituo vya kazi
inapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya www.moh.go.tz. na tovuti ya
Taasisi ya Benjamin Mkapa www.mkapafoundation.or.tz.
Aidha tunapenda kuwafahamisha wote waliopangiwa kazi kuwa, ajira hizi ni
za mkataba na zinasimamiwa na Taasisi ya Mkapa kupitia Mradi wa
Kuimarisha Mifumo Stahimilivu na Endelevu ya Afya (RSSH). Kabla au
baada ya kukamilika kipindi cha mkataba, waajiriwa wote katika mradi tajwa
wanaweza kupata nafasi ya kujiunga katika ajira za Utumishi wa Umma
kulingana na taratibu za Serikali za Ajira iwapo nafasi za ajira zitapatikana.
Limetolewa na:-

Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto
kwa ushirikianao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa

Opening Date: 29th September 2021

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *